Waamimi 279 wa Parokia ya Makutano wapokea  Kipaimara .

Waamimi 279 wa Parokia ya Makutano wapokea Kipaimara .

Na Idara ya Mawasiliano
Waamini hao wameaswa kuwa waaminifu katika mambo ya familia, kijamii na hata katika Kanisa ambapo anasema unapofanya jambo lisilo la uaminifu ni sawa na mtu anayetenda dhami anayoifahamu.
Naibu wa Askofu wa Jimbo hilo ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa homilia Septemba 3,2025 katka Parokia hiyo ,Misa iliyohudhuliwa na waamini wa vigango vote vinavyounda Parokia hiyo.
Paroko wa Parokia hiyo Padri Andrea Tungaraza amemshukuru Naibu wa Askofu kwa kufika na kuwaimarisha waamini hao kwani ni takribani miaka mitano toka Sakramenti Takatifu ya mwisho itolewe katika Parokia hiyo.