HOSPITALI YA KOWAK YAZINDUA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI.

HOSPITALI YA KOWAK YAZINDUA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI.

Na Idara ya Mawasiliano
Hospitali ya Kowak iliyopo Jimbo Katoliki la Musoma imezindua rasmi Jengo la kuhifadhia maiti (mortuary) 12 kwa mara moja baada ya huduma hiyo kutokuwepo katika hospitali hiyo .
Akizungumza na Diocese of Musoma online Tv mara baada ya kubariki jengo hilo ,Paroko wa Parokia hiyo Padri Cleophas Sabure amesema moja ya changamoto kubwa walikuyokuwa wanakabiliana nayo wahudumu wa afya wa hospitali hiyo ilikiwa ni ukosefu wa chamba maalumu cha kuhifadhi ndugu zetu mara baada ya kuondoka hapa duniani.
“Hospitali imefanya jitihada kubwa sana kujenga chumba hiki chenye uwezo wa kuhifadhi miili 12 kwa wakati mmoja,awali walikuwa wanasafiri umbali mrefu sana kuwapeleka kuwahifadhi ndugu zetu utegi au Shirati hali ambayo ilikuwa inaongeza gharama kubwa ya usafiri lakini kwa sasa watakuwa hawatumii gharama kuwasafirisha ndugu zetu kwa ajili ya kuwahifadhi wakati wanajiandaa na mazishi “amesema Padri Sabure.
Lucy Jacob na Joan Ojwung’ wameushuku uongozi wa hospitali ya Kowak kwa kufikiria na kuamua kujenga chumba hicho ambacho kitatumika kuwahidhi ndugu zetu kwa muda baada ya kuondoka hapa duniani.
Na Idara ya Mawasiliano