WAAMINI WATIMIZA AHADI YA GARI KWA ASK.MICHAEL MSONGANZILA

WAAMINI WATIMIZA AHADI YA GARI KWA ASK.MICHAEL MSONGANZILA

Na Idara ya Mawasiliano
Mhashamu Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo la Musoma amepokea Zawadi ya gari ambalo waamini walimuahidi wakati wa Jubilei yake ya miaka 40 ya Upadre iliyofanyika mwaka jana 2024.
Akipokea gari hilo na kulibariki Septemba 16, 2025 Askofu huyo amewashukuru Mapadre, Watawa na Waamini wote wa ndani na nje ya Musoma kwa zawadi hiyo itakayomsaidia katika shughuli mbalimbali za Kichungaji.
“Asante sana watu wote kwa majitolea yenu kwa ajili ya kunisaidia katika shughuli zangu mbalimbali za u hung uchungaji, mlipotoa Mwenyezi Mungu awabariki”amesema Askofu Msonganzila.